Kisa Dakika Tisini…Ajibu, Kamusoko Wawekewa Ulinzi Mkali

 

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.

BENCHI la ufundi la Majimaji limewapa maagizo maalum mabeki wa timu hiyo chini ya kitasa wao, Tumba Sued kuhakikisha wanatumia mbinu zao ili kuizima safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo inaongozwa na Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu, wasipate bao kwenye mchezo wao wa wikiendi hii.

Majimaji ambao wanafundishwa na Peter Mhina akisaidiwa na Habibu Kondo, watakuwa wenyeji wa Yanga wikiendi hii kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma. Mara ya mwisho vikosi hivyo vilipokutana uwanjani hapo Yanga walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Deus Kaseke.

Haruna Niyonzima akimtoka Kamusoko.

Kikizungumza na Championi Jumatano, chanzo toka ndani ya timu hiyo kimesema kuwa wameiona safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji na kuona safu yao ya ushambuliaji ndiyo inaibeba timu hiyo ndiyo maana wameweka mikakati maalumu ya kuhakikisha hawafurukuti mbele yao.

 

“Yanga tumewaona tulivyokuwa hapa Njombe kwenye mchezo wao na Njombe Mji na tumebaini kuwa uzuri wao na uhai wa timu upo kwenye maeneo mawili, eneo la kiungo ambapo msumbufu ni yule Thaban Kamusoko na ushambuliaji ambapo yupo Ajibu.

“Sasa baada ya kuyabaini hayo tumeandaa mkakati mzito kuhakikisha tutakapocheza nao basi hawaleti madhara.

“Tayari walinzi wetu wameonyesha dalili kubwa ya kuelewa kile ambacho tunawapa ili tu wapinzani wetu hao wasiweze kutufunga,” kilisema chanzo hicho.

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment