The House of Favourite Newspapers

KISA DENI, FAMILIA YAFURUMUSHWA KWENYE NYUMBA

Noja Kinyamagoa ambaye alitumia nyumba hiyo ya jamaa zake kama dhamana ya mkopo.

FAMILIA ya mkazi mmoja wa Keko Magurumbasi Jijini Dar, Noja Yohana imejikuta katika wakati mgumu na kutupiwa vyombo nje baada ya jamaa wa familia hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Joashi Kinyamagoa kukopa milioni nne kwenye benki moja hapa jijini na huku akitumia nyumba hiyo kama dhamana kisha kushindwa kurejesha mkopo huo.

Mtoto wa mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina la Faines Yohana akielezea kilio chake.

Imeelezwa kuwa, Kinyamagoa alikopa pesa hizo na kulipa marejesho kadhaa lakini alishindwa kumaliza deni lote kwa wakati hivyo nyumba hiyo akapigwa mnada na kuuziwa mteja mwingine kwa shilingili milioni saba.

Bibi Elena John ambaye ni dada wa mwenye nyumba na mkazi wa nyumba hiyo naye akielezea jinsi wanavyoondolewa kwa nguvu kwenye nyumba hiyo huku wengine wakiwa kazini.

Baada ya nyumba hiyo kununuliwa familia hiyo imelalamikia kitendo cha kutupiwa nje vitu vyao na kutaka kubomolewa nyumba yao wakati na wao wamefungua kesi kupinga nyumba yao kuuzwa.

Hivi navyo vilitupwa nje.

Aidha, Kinyamagoa akizungumza na www.globalpublishers.co.tz amekiri kuchukulia mkopo kwa nyumba hiyo na baada ya kuchelewesha marejesho ndipo ikapigwa mnada lakini alilalamikia nyumba hiyo kuuzwa haraka bila kumvumilia ajitafute ili akalipe deni hilo.

Baadhi ya vitu vikiwa vimetupwa nje na watu wanaodaiwa kuwa mabaunsa wa mnunuzi.

 

Moja ya mabanda ya nyumba hiyo nayo vitu vikiwa vimetupwa nje.
Baadhi ya wanaoishi nyumba hiyo wakishindwa kupika wala kuendelea na chochote kufuatia kizaazaa hicho. 

 

Mshuhuda wakifuatilia kinachoendelea.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL  

Comments are closed.