The House of Favourite Newspapers

KISA DENI LA NYWELE, AMBER LULU AFUNGIWA SALUNI

UBUYU nao siku zote una staili yake ya kuula. Ubuyu mwingine unauacha tu mdomoni kisha unatema mbegu huku mwingine unamun’gunya hadi mbegu hadi zinapasuka.

Ubuyu uliotufikia ni kwamba msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri kupitia wimbo wake wa Jini Kisirani, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ anadaiwa kufungiwa saluni siku nzima bila kutoka, kisa kikiwa ni deni la fedha za nywele za wigi anazodaiwa.

Kwa mujibu wa msambaza ubuyu huo, msanii huyo alikopa nywele za shilingi milioni moja na laki tano kwa dada mmoja aitwaye Bonita, ambaye ana saluni yake maeneo ya Mwananyamala- Komakoma jijini Dar.

Ilidaiwa kuwa, tangu Amber Lulu akope, ulipita muda mrefu huku akimzungusha Bonita.

“Tangu Amber Lulu akope hizo nywele alikuwa haendi tena kwa Bonita, lakini pia hata akipigiwa simu alikuwa hapokei kabisa.

AMBER LULU AFUNGIWA SALUNI

“Kwa kifupi alimkatia kabisa mawasiliano Bonita. Afadhali angemwambia kuwa hana fedha angejua au hata angempa muda wa kulipa, lakini alikuwa akimjibu vibaya na kumkatia kabisa mawasiliano hadi alipoingia kwenye 18 na kujikuta akifungiwa ndani ya saluni,” alidai msambaza ubuyu huo.

Baada ya Ijumaa Wikienda kuunyaka ubuyu huo, lilianza kwa kumtafuta Bonita ambaye ni mmiliki wa saluni hiyo na kumuuliza kuhusiana na madai ya kumfungia Amber Lulu ndani ya saluni kwa sababu ya kushindwa kulipa wigi ambapo mambo yalikuwa hivi;

BONITA SASA

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Bonita?

Bonita: Salama kabisa, karibu.

Ijumaa Wikienda: Kuna madai kuwa ulimfungia Amber Lulu ndani ya saluni yako, kisa unamdai wigi la shilingi milioni moja na nusu, je, hii ishu ikoje?

Bonita: Ni kweli na tena bado hajailipa. Aliniambia angelipa badaa ya kumuachia, lakini bado hajalipa. Ila nimeshamtangazia vita popote nitakapomuona ninaye.

Ijumaa Wikienda: Sasa nywele za milioni moja na nusu ni wigi moja tu?

Bonita: Ndiyo, lile wigi ni Peruvian ndefu hadi kwenye makalio.

Ijumaa Wikienda: Sasa umeshaenda Polisi kumshtaki?

Bonita: Hapana, huyu ninadili naye mwenyewe, mbona ninammudu tu mimi?

BOFYA HAPA KUMSIKIA AMBER LULU

Baada ya kumsikia Bonita, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Amber Lulu ili naye ayafungukie madai hayo ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Amber Lulu inasemekana kuwa unadaiwa nywele na Bonita na hutaki kulipa pamoja na kwamba kuna siku alikufungia ndani ya saluni siku nzima!

Amber Lulu: Huyo dada anatafuta kiki sana kupitia jina langu.

Ijumaa Wikienda: Je, ni kweli anakudai hizo nywele?

Amber Lulu: Nimeshakwambia huyo dada anatafuta kiki na mimi sitoi kiki ng’o, aendelee tu kunifuatilia atazipata tu fedha zake.

 

UBUYU ULIYONYOOKA | Na Imelda Mtema | SIMU; +255 754 021 301

Comments are closed.