The House of Favourite Newspapers

Kisa Jide,Nandy zuchu yamkuta mazito

0

MREMBO anayekuja kwa kasi kunako anga la Bongo Fleva, Zuhura Kopa ‘Zuchu’ yamemkuta mazito kufuatia shabiki mmoja kutaka asilinganishwe uwezo wake na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide na Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’.

Iko hivi, ishu ilianzia kwenye ukurasa wa Twitter baada ya shabiki mmoja anayejiita Lavie kwenye mtandao huo kuonesha mtazamo wake kuwa Zuchu bado ni mdogo sana kimuziki na asilinganishwe hata kidogo na wasanii hao waliomtangulia hususan Jide. “Ukweli ni kwamba, Zuchu bado saana kwenye game ya music, sema kinachombeba ni label aliyopo WCB. Kumlinganisha Zuchu na Nandy au na Lady Jaydee, ni utovu wa nidhamu,” aliandika Lavie.

Baada ya kuandika hivyo, Jide ali-like ujumbe huo kuonesha kwamba anakubaliana na kilichoandikwa na Lavie na hilo sasa ndilo likawa kosa baada kipande hicho cha maneno kutupiwa kwenye mitandao mingine ya kijamii na watu kuanza kutoa maoni yao ambayo dhahiri ‘yalimpiga’ Zuchu. “Samahani mimi ni mgeni…Zuchu ni label au sabuni au nini samahani, sifahamu chochote nimepotea njia.”

“Mkuu! Zuchu mlinganishe na Ebitoke.” “East Africa Jide hafanani na kikaragosi chochote cha jinsia yake, Jide ni komando na msanii mzuri kweli kweli.”“Wewe unapambanisha Barcelona vs Njombe hahahahahahahahah.” Hayo ni baadhi ya maoni ambayo yalimshambulia vibaya Zuchu. Lakini hata hivyo, wapo baadhi ya wadau waliomtetea msanii huyo mchanga kwenye gemu.

“Ukiona wengi wanamfananisha na kumpambanisha Zuchu na wasanii wakubwa, basi jua she’s more talented kiasi kwamba watu washaanza kumuogopa. Wakati Nandy na Maua Sama wanapanda kwenye charts, hakuwepo mtu wa kuwapambanisha, leo anatoka Zuchu limeibuka kundi la haters ambao kila siku ni kumponda na kumpambanisha na wasanii wakike waliotangulia,” mmoja wa wadau alimtetea na kuongeza:

“Hizi ni ishara kuwa Zuchu ni tishio kwao, pia wasichojua kuwa Zuchu alikuwa msanii aliyekamilika tangu akiwa anaingia Wasafi 4yrs ago, amekaa pale akisoma game na strategy za ku-win, pia kuongeza maujuzi lakini angeweza kutoka enzi Nandy ni mbichi kwenye game.

“Watu wanatakiwa kutulia kumpa nafasi Zuchu afanye kile akipendacho kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine kumu-attack means ni tishio kwa mashabiki wa wasanii kupambanishwa, na bado Zuchu ataendelea kuwanyima usingizi, bado mapema mno kulalamika.”

Zuchu kwa sasa anasumbua na ngoma kali ya Nisamehe lakini kama hiyo haitoshi, ngoma zake zilizotangulia kama Wana, Raha na Kwaru zote zimekimbiza vibaya na kumfanya awazidi kinoma Jide na Nandy kwa watazamaji (views) YouTube.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Leave A Reply