The House of Favourite Newspapers

KISA KAULI YA UFISADI, AKAUNTI ZA RAIS KENYATTA ZAFUNGWA

 

AKAUNTI  za mitandao ya kijamii za Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta,  za  Facebook, na Tweeter,  zimefutwa kwenye mitandao hiyo siku ya Ijumaa, Machi 22, leo asubuhi.

 

Akaunti hizo zimefutwa ikiwa ni muda baada ya kutoka ujumbe  ambao ulikuwa unasema kwamba hakuna atakayepona kwenye vita dhidi ya ufisadi.

 

 

“Kama wewe ni fisadi tutapigana na wewe. Unaweza ukawa dada yangu, kaka au mtu wa karibu na mimi kwenye siasa. Siwezi kushikamana na kikabila au hali katika jitihada yangu ya kuondoka kwa taifa lenye umoja na nitaendelea kuimarisha umoja wa Kenya” Yalisomeka maneno yaliyoandikwa Tweeter

 

 

Nzioka Waita mkuu wa wafanyakazi wa ofisi ya rais huyo amesema kwamba akaunti hizo zimezuiliwa kwa muda.

“Hii ni kutokana na kuingiliwa kiharamu kwa akaunti rasmi za mitandao ya kijamii za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta. Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamii zimesimamishwa kwa muda kwa ajili ya kuruhusu kufanyika marekebisho yanayotakiwa,” alisisitiza Waita.

Comments are closed.