The House of Favourite Newspapers

Kisa kuokoka Kajala akejeliwa

1

Kajala-Masanja-akiwa-katika-poziKajala Masanja

BAADA ya kukiri katika gazeti hili kuwa ameamua kuokoka na kumrudia Mungu, mrembo kunako filamu za Kibongo, Kajala Masanja amekejeliwa na baadhi ya watu wake wa karibu.

Akizungumza na Amani Kajala alisema kitendo cha kuokoka kimegeuka kama kejeli kwa marafiki zake ambapo wengi humcheka lakini anaamini kabisa siyo akili zao bali shetani anataka kuwatumia ili aanguke.

“Kuna ambao wananicheka kicheko kikubwa kabisa baada ya kusikia kuwa nimeamua kumfuata Yesu na wengine kunikejeli lakini mimi sina neno naamini kabisa ni nguvu ya shetani ili nirudi nilikotoka, nawaambia tu watakuwa wamechelewa sana,” alisema Kajala.

1 Comment
  1. digna says

    Hongera sana kwa kujitambua mapema. na kumrudia Bwana Yesu Kristu umechagua jambo lililo bora hapa duniani. wala usiwe na wasiwasi na wanaokucheka kwa sababu wangejua utamu wa Yesu wangeacha yoooote na kumfuata. endelea kuwaombea tu wataujua ukweli. Tumsifu Yesu Kristu Milele daima Aminaaaaaaaaaaa.

Leave A Reply