The House of Favourite Newspapers

Kisa kushindanishwa na Gigy… Pam D Atokwa Povu la Mwaka

0
Gigy Money.

MWANADADA kiwango kwenye Bongo Fleva, Pamela Daffa `Pam D’ amesema anakerwa na baadhi ya mashabiki wa muziki wanaomshindanisha na mwanamuziki mwenzake ambaye pia ni muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford `Gigy Money’ kwamba kushindanishwa huko ni kushushiwa heshima.

Pam D.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Pam D anayekimbiza kwenye gemu na Wimbo wa Ngoma Droo alifunguka kuwa, Gigy kwake ni msanii anayeanza na kamwe si mwanamuziki wa kumshindanisha naye.

”Mambo ya kushindanishwa na Gigy sipendi, kila mmoja anafanya muziki wake na ana mashabiki wake, kwanza huyo Gigy hata tukiwekwa naye jukwaani namfunika, kwa hiyo watu waache kama nilivyo na si kunishindanisha kusipokuwa na mpango…” alisema Pam D.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI

 

JWTZ Wakizika Miili ya Watoto Waliolipukiwa Bomu Monduli

Leave A Reply