Kisa kutoalikwa, Wema asusia keki

WEMA2Staaasiyeishiwa vituko Bongo, Wema Sepetu.

NaMusa Mateja, Risasi Mchanganyiko
STAA asiyeishiwa vituko Bongo, Wema Sepetu juzikati aligonga tena vichwa vya habari baada ya kukataa kula keki ya sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Chidy Mapenzi, kwa kile kilichodaiwa kuwa hakualikwa.

Chanzo chetu cha kuaminika kinadai kuwa wakiwa katika mitoko yao ya kila siku, Wema, Aunt Ezekiel na Kajala walijikuta wameibukia Club Billicanas kwa ajili ya kujirusha. Wakiwa ukumbini hapo, ghafla muziki ulizimwa na tangazo kutolewa kuwa siku hiyo, Chidy Mapenzi alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa yaani bethidei.

Baada ya tangazo hilo, Chidy alipanda jukwaani na baadhi ya marafiki zake wakaitwa ili kula keki iliyoandaliwa, lakini alipoitwa Wema, alikataa kwa madai ya kutoalikwa rasmi katika shughuli hiyo.

“Watu walimshangaa sana Madam, alipoitwa akakataa katakata, na hata Kajala naye alipoitwa alienda lakini akakataa kula keki, akaibeba na kumpelekea Wema aile, bado akakataa,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Wema ili kuzungumzia suala hilo lakini mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.


Loading...

Toa comment