KISA LAANA QUEEN DARLEEN AMWANGUKIA BABA’KE

Related image

Mwana­hamisi Abdul ‘Queen Darleen’

BAADA ya kuwa kwe­nye mgogoro kwa muda mrefu na baba yake mzazi, Abdul Juma ‘Baba D’, ili kukwepa laana ya mzazi, hati­maye msanii wa Bongo Fleva, Mwana­hamisi Abdul ‘Queen Darleen’ ametambua umuhimu wa wazazi na kuamua kumfuata na kumuomba msa­maha.

Akizungumza na Iju­maa Wikienda, Baba D alisema ni kweli awali ali­kuwa na ugomvi mkub­wa na Queen Darleen na ikafikia hatua mpaka ya kumtamkia maneno mazito kuwa hata akifa binti yake huyo asimzike ila anamshukuru Mungu kwamba mwanaye huyo ametambua makosa yake na kujirudi.

“Haya ni mambo ya kawaida tu katika familia, ni kweli mimi na Queen Darleen tulikuwa na ugomvi mkubwa mpaka ikafikia hatua nikamtamkia maneno mabaya kwamba iki­tokea nimefariki dunia asije kunizika, jambo ambalo si zuri, lakini ameyatambua ma­kosa yake, akaja kuniomba msa­maha na mimi nikamsamehe kwa moyo mmoja,” alise­ma Baba D.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Toa comment