Kisa Manula, Kahata Apewa Mil 200

BAADA ya uongozi wa Al Merrikh ya Sudan kugonga mwamba kwenye dili la kumnasa kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula, hatimaye sasa dili lao wamelielekeza kwa nyota mwingine wa Simba, Francis Kahata.

 

Tayari Kahata ameshaaga kwa mashabiki na wachezaji wenzake wa Simba, hii ni baada tu ya mkataba wake kumalizika, huku tayari akiwa amepata ofa ya zaidi ya milioni 200 kwa Al Merrikh ya Sudan ambapo imefikia hatua hiyo baada ya Simba kugoma kuwauzia Manula.

 

Ikumbukwe tu kuwa takriban miezi mitatu huko nyuma timu ya hiyo ya Sudan, kupitia kwa rais wao, Adam Sudacal, ilikuwa kwenye nia ya kutaka huduma ya Manula kiasi cha kuamua kutoa ofa ya zaidi ya Sh milioni 200.

Hii ni baada ya kocha wa Waarabu hao Lee Clark, kuukubali utendaji kazi wake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambapo Simba waliondolewa hatua ya robo fainali na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3.

 

Chanzo chetu kutoka Simba kimeliambia Championi Jumatano kuwa, hadi Kahata anaagana na Simba tayari alikuwa na ofa mkononi ya kuitumikia Al Merrikh ya Sudan hii ni baada ya uongozi wa Simba kugoma kuwauzia Manula jambo ambalo limewapelekea kurejesha nia yao kwa Kahata na tayari wameshazungumza na muda wowote atakuwa sehemu ya kikosi chao.

 

Achana na habari za Manula sasa mambo ni Kahata na Al Merrikh, jamaa baada ya sisi kushindwana nao sasa wameamua kumalizana na Kahata, jambo ambalo limeufanya hata uongozi wetu kushindwa kufanya makubaliano mapya na Kahata ili aongeze mkataba mpya maana jamaa wamempatia dau la zaidi ya milioni 200,” kilisema chanzo hicho.

Stori: Musa Mateja, Dar es SalaamTecno


Toa comment