Kisa Manula, Shabiki Apigwa Faini ya Elfu 20 Simba

KATIKA hali isiyotarajiwa, kwenye mazoezi ya Simba, kocha mpya wa makipa wa timu hiyo raia wa Afrika Kusini, Tyron Damos, alimkamata shabiki mmoja akirekodi mazoezi aliyokuwa akimpa kipa wake Aishi Manula na kuamuru shabiki huyo alipe faini ya Sh 20,000.


Kwenye mazoezi hayo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO arena, Bunju Dar es Salaam, Simba waliruhusu watu mbalimbali kurekodi mazoezi hayo kwa dakika 15 tu kabla ya kuzuia kurekodi
mazoezi ya kimbinu.

 
Licha ya zuio hilo shabiki
mmoja aliendelea kurekodi na kumfanya kocha huyo Msauzi kumshtukia ambapo
alisimamisha mazoezi na
kumfuata shabiki huyo na kumwambia anapaswa kulipa faini ya Sh 20,000 kwa kukiuka maelekezo.

Championi Ijumaa, lililokuwa uwanjani hapo lilishuhudia kocha Tyron akisema: “Nimekuona ulikuwa ukirekodi programu zetu za kiufundi nilizokuwa nampa Manula na kwa kuwa hiyo ni kinyume cha maelekezo basi utapaswa ulipe faini ya shilingi 20,000.”


Mwishoni kocha huyo
alianza kutabasamu na kumwambia shabiki aliyekuwa akirekodi kuwa alikuwa anamtania, na kumtahadharisha kuwa asiendelee kufanya hivyo.

STORI: JOEL THOMAS,Dar es Salaam701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment