The House of Favourite Newspapers

Kisa Mtoto wa Mobeto, Zari Atoa Mapovu Balaa

0
Zarina Hassan ‘Zari’

LILE sakata la mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, Abdulatif Nasibu kuzua utata, kila mmoja akiwa na shauku ya kumjua baba wa mtoto huyo, hatimaye ukweli umefahamika baada ya msanii wa Bongo Fleva aliyekuwa akihusishwa naye kwa muda mrefu, kujitokeza hadharani na kukiri kwamba yeye ndiye baba halisi wa mtoto huyo, jambo lililoamsha hasira kali kwa mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’.

Zari ambaye amezaa naye watoto wawili, muda mfupi baada ya msanii huyo kusikika kwenye kituo kimoja cha redio na runinga akikiri kwamba mtoto huyo ni wake, na kwamba amekuwa akimhudumia kwa siri huku akisherehesha kwamba alishamwambia Zari na akakubaliana na hali halisi, mwanamama huyo amekuja juu na kutoa mapovu si ya nchi hii.

Hamisa Mobeto.

“Hahahaha unajidanganya, unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na maneno yako,” Zari aliandika ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Snapchat na kuongeza:

“Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndiyo maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda u-google kuhusu ‘defamation of character lawsuit’, usinijaribu.”

Kauli hiyo ya mwanamama huyo, imezua gumzo upya kwa sababu inaonesha dhahiri kwamba alichokisema msanii huyo, kwamba Zari anafahamu kuhusu sakata hilo na walishalimaliza, ni uongo.

Leave A Reply