The House of Favourite Newspapers

Kisa Mwanaye, Hamisa Mobeto Amlilia Lulu!

0


Mwanamitindo anayebamba vilivyo na kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika nchi mbalimbali, Hamisa Mobeto, kwa mara ya kwanza ameongea kuhusu hukumu ya kifungo cha miaka miwili inayomkabili muigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambapo amesema amehuzunishwa na kilichompata kwani alikuwa ni mlezi mzuri wa mtoto wake wa kwanza, Fantasy, ambaye amezaa na mfanyabiashara Majizzo anayebanjuka kimapenzi na Lulu kwa sasa.

“Kitu ambacho naweza kuongea kuhusu Lulu, kwa sasa ni kwamba anatakiwa kuwa jasiri, Mwenyezi Mungu anawapa mitihani wanajeshi wake ambao anajua wanaweza kuimudu, japo kwa upande wangu najisikia vibaya kwa sababu zamani nilikuwa huru hata kusafiri najua mtoto yupo kwa baba yake na Lulu watamuangalia vizuri, kama familia tumeumia sana,” amesema Mobeto.

Na Isri Mohamed/ GPL

Leave A Reply