The House of Favourite Newspapers

Kisa Obama, Trump Agoma Kuzindua Ubalozi Wake Uingereza

Ndani ya jengo hilo.

Rais wa Marekani, Donald John Trump amekataa safari yake ya kwenda nchini Uingereza ambapo mbali na mambo menginine ambayo angefanya, angezindua jengo jipya la Ubalozi wa Marekani nchini Uingereza.

 

Jenso hilo kwa nje.

 

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Trump alisema kuwa mtangulizi wake, Rais Obama aliuza jengo la awali la ubalozi wa nchi hiyo kwa bei chee, ili kujenga jengo jingine tena sehemu ambayo si nzuri.

 

Ndani ya jengo.

 

Uamuzi wa kuuza jengo hilo la zamani ulifanya wakati wa utawala wa Rais George W Bush, na kilichopelekea uamuzi huo ni kutokana na sababu za kiusalama.

Jengo jipya la ubalozi wa Marekani lina ghorofa 12 likiwa limepambwa kwa vioo vingi. Jengo hilo limegharimu TZS 2.2 bilioni na linatarajiwa kufunguliwa rasmi Januari 16 mwaka huu.

Litakuwa ndio jengo la ubalozi la ghali zaidi kuwahi kujengwa.

Comments are closed.