The House of Favourite Newspapers

KISA PIERRE SHILOLE YAMKUTA

YAMEMKUTA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kujikuta akishambuliwa kwa maneno makali na wananzengo kutokana na kauli yake ya kumuita Piere kuwa ni mtu wa hovyo.

 

Shilole alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika ‘event’ ya Tokomeza Ziro ya mwanadada Jokate Mwegelo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo alipopewa nafasi ya kuzungumza, alimzungumzia Piere kuwa ni mtu wa hovyo.

Baada ya kauli hiyo, Shilole alikula za uso ileile hali iliyomlazimu kuomba radhi lakini hata hivyo bado mashabiki waliendelea kumchana tu.

Comments are closed.