The House of Favourite Newspapers

Kisa Simba, Matajiri Wavamia Kambi Mbeya

0

WAKATI kikosi chao kikitua jana mchana mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara, vigogo matajiri wa Yanga wenyewe leo Ijumaa wanatarajiwa kuungana na kikosi hicho katika kuongeza morali ya wachezaji na kupangua hujuma za wapinzani wao.

 

Yanga ipo kileleni ikiongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 44, kesho Jumamosi saa kumi jioni inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuvaana na Mbeya City mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa Timu hiyo hadi hivi sasa ikicheza michezo 18 ya ligi haijafungwa, imeshinda 13 huku ikitoa sare mitano waliyoicheza katika msimu huu.Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, msafara huo utamjumuisha Makamu Mwenyeki wa Kamati ya Usajili na Mashindano ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said.

Mtoa taarifa huyo alimtaja tajiri mwingine ni Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Thobias Lingalangala ambaye amekuwa akisaidia kuchangia fedha za usajili kwa wachezaji.Aliongeza kuwa wengine ni Rogers Gumbo na Davis Mosha ambao watawawakilisha matajiri wenzao, Abdallah Bin Kleb na Seif Magari ambao waliokuwepo kwenye Kamati ya Mipango ya Ushindi ya timu hiyo ambao kazi yao ni kuongeza morali ya wachezaji uwanjani ili kuhakikisha wanabeba taji la ligi msimu huu.

 

“Upo Umoja wa Kamati ya Mipango na Ushindi wa Yanga ambao umeundwa tangu kuanza kwa msimu huu ambao wenyewe lengo lao ni kubeba ubingwa wa ligi.“Wenyewe kazi yao ni kufanikisha ushindi kwa kuwapa morali wachezaji wao na kupangua hujuma za wapinzani wao wanaokutana nao katika mchezo husika wa ligi.

“Hivyo, matajiri hao kesho (leo) asubuhi watapanda ndege kuelekea Mbeya kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi katika mchezo huo mgumu waliopanga kuondoka na pointi tatu na lengo ni kuendeleza rekodi ya kutopoteza,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Lingalangala ambaye anaunda kamati hiyo mpya kuzungumzia hilo alisema: “Nikiwa mmoja wa wajumbe wa Yanga, sisi kama uongozi tunataka kuona timu inafikia katika hoteli nzuri hiyo yote katika kuwapa mazingira mazuri wachezaji ya kupata ushindi.“

 

Hivyo, viongozi tutakwenda huko kwa ajili ya kuwaongezea nguvu na morali wachezaji wetu ili kuhakikisha tunapata ushindi na mimi nitakuwepo sehemu ya msafara huo.”

Stori: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply