The House of Favourite Newspapers

Kisa Super Cup, Simba Yafumua Benchi La Ufundi

0

KATIKA kuhakikisha wanaadika historia ya kufanya makubwa katika mashindano ya CAF Super Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kwa mara ya kwanza mwezi Agosti mwaka huu, uongozi wa Simba umefichua kuwa utafanya maboresho makubwa ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Simba ndiyo timu pekee kutoka Tanzania ambayo imechaguliwa kushiriki mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Agosti mwaka huu na kushirikisha timu nane ambazo ni Mamelodi Sundowns, Petro de Luanda, TP Mazembe, Horoya, Wydad Atheltic Club, Simba SC, Esperance de Tunis na Al Ahly.

Akizungumzia maandalizi ya Simba kuelekea mashindano hayo ya Super Cup, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema: “Super Cup ni mashindano makubwa sana kuwahi kuanzishwa Afrika na hii inathibitishwa na ubora wa timu shiriki. Tunakwenda kushindana na Wydad Casablanca, Esperance, TP Mazembe, Al Ahly, Mamelodi Sundowns.

“Katika hali kama hii ni lazima tuhakikishe tunakuwa na uzito wa kutosha kulinganisha na washiriki wenzetu hivi karibuni tunatarajia kutangaza maboresho ya benchi letu la ufundi ambapo tutamtangaza Mkurugenzi wa michezo na watu wa Sports Science.”

Stori na Joel Thomas

VITUKO vya STANI BAKORA na MKALI WENU KWENYE NDOA ya DULLA MAKABILA – ”WATAZAA MWARABU”…

Leave A Reply