The House of Favourite Newspapers

Kisa Sure Boy, TFF Yawaonya Azam

0

BAADA ya uongozi wa Azam FC, kuwasimamisha wachezaji wao, Aggrey Morris, Aboubakary Salum ‘Sure Boy’ na Mudathir Yahaya kwa muda usiojulikana, Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limeiagiza timu hiyo
kutoa adhabu ya muda maalum.

 

Wachezaji hao walisimamishwa hivi karibuni na timu hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na kosa la utovu wa nidhamu.


Chanzo chetu kutoka Azam FC,
kimeliambia Championi Jumatano kuwa, TFF imeingilia sakata hilo na kuwataka
Azam kutoa adhabu ya muda maalum
kwa wachezaji hao ili waweze kurejea kwenye majukumu yao ya kawaida na kama hawataki basi wawaruhusu kwenda kutumikia timu zingine na si kuua vipaji vyao.


“Ni kweli TFF imewataka viongozi
wa Azam kutoa adhabu maalumu kwa wachezaji hao na kama hawawahitaji
basi ni vyema wawafukuze ili wakatafute
sehemu nyingine ya kucheza endapo kama bado wana malengo nao basi
wawape adhabu ya muda maalumu.”


Championi lilimtafuta Meneja Mwajiri
wa Azam FC, Khamis Ally ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema: “Nilikutana na viongozi wa TFF wakati nikielekea Zanzibar kwenye shughuli zangu za kazi wakaniambia wamenitumia barua nikirejea Dar es Salaam nitaisoma ili tuweze kuwajibu.”


Aidha Championi lilimtafuta
Mwenyekiti wa Chama cha Wanamichezo nchini, (SPUTANZA), Mussa Kisoki ili
azungumzie pia sakata hili alisema:


“Siyo sisi tuliotuma hiyo barua Azam
ila ni TFF wenyewe maana hata kwenye kanuni zetu jambo hilo lipo kwa kuwa huwezi kumpa adhabu mchezaji isiyoeleweka lini mwisho wake ila nimefurahia kuona wachezaji husika
wakienda kuwashitaki TFF maana ni haki
yao hata kama wamekosea.

Stori: Musa Mateja na Careen, Oscar, Dar es Salaam

Leave A Reply