The House of Favourite Newspapers

Kisa ujauzito wa Ali Kiba, Jokate aasi kanisani

IMG-20151118-WA0010Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo.

Gladness Mallya na Mayasa Mariwata
IMEVUJA! STAA wa muziki na mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amedaiwa kuasi kanisani kisa kikitajwa ni kutokana na ujauzito alionao, unaohusishwa na mkali wa Bongo Fleva, Abdul Saleh Kiba.

Chanzo makini cha gazeti hili ambacho kiko karibu na mwanadada huyo, kilisema kwa muda sasa amekuwa haonekani kanisani kama awali, na hata kwenye kwaya aliyokuwa akiimba ndani ya kanisa analosali la St. Peter lililopo Oystebay jijini Dar, haonekani.

“Yaani Jokate ujauzito alionao unamsumbua sana, ameacha hata na kuimba kwaya, kanisani haonekani kama ilivyokuwa zamani, pia hali hiyo inachangiwa na kwamba anaona aibu amebeba mimba nje ya ndoa, yaani hajaolewa ndiyo maana mara nyingi haendi kanisani,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo waandishi wetu walifunga safari mpaka kanisani kwa ajili ya kuonana na kiongozi wa kwaya aliyejulikana kwa jina moja la Catherine, ambapo walimkosa na kufanikiwa kuzungumza naye kwa njia ya simu baada ya kupewa namba zake.
“Jokate kwa sasa haimbi kwaya, amesitisha lakini sijui sababu ni nini,” alieleza kwa kifupi baada ya kuulizwa juu ya upatikanaji wa mrembo huyo maarufu kama Kidoti.
Ili kuleta mzani wa habari, Jokate ambaye ni mwandani wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba naye alitafutwa na kuelezwa habari hizo, ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Ni kweli siimbi kwaya mwaka sasa, ila kanisani sijaacha kwenda na siwezi kuacha kwenda na bado kazi za kanisa nyingine nafanya, sijaacha kwa sababu ya mimba bali ratiba zangu tu zilikuwa ngumu.”

Comments are closed.