The House of Favourite Newspapers

Kisa Vicoba… Mwanamke akombwa kila kitu

0

Morogoro: Hapana chezea Vicoba! Mwanamke Hellena Haule ‘Mama Wawili’ ambaye ni fundi wa nguo, kwa sasa analala chini baada ya kudaiwa ‘kuchikichia’ fedha za Vicoba hivyo wenzake kutia timu chumbani kwake na kumkomba kila kitu ikiwemo cherehani anayofanyia kazi.

Tukio hilo la fedheha lilijiri mchana kweupe mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mwanamke huyo Mtaa wa Kingo, Msufini mjini hapa.

Akizungumza na Wikienda, mmoja wa wanakikundi, Halima Juma alisema kuwa Hellena ni mwanachama mwenzao wa Kikundi cha Vicoba cha Tuungane na kwamba alichukua mkopo wa Sh. milioni 2.2 tangu Juni, mwaka jana ambapo deni hilo alitakiwa kulimaliza Desemba lakini akashindwa kufanya hivyo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kingo, Misufini, Mwajuma Ndege alikiri kupokea malalamiko hayo na kusema: “Hellena ameshindwa kulipa deni hilo baada ya biashara yake ya ushonaji kumuendea vibaya hivyo kwa kuwa kuna ‘document’ alizosaini, wenzake wameamua kuchukua vitu vyake vyote zikiwemo fenicha na cherehani.”

Kwa upande wake, Hellena alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema kwa sauti ya upole: Sina jinsi, maisha yameniendea kombo, nimekopa, nimefanya biashara, nikapata hasara, nimewaomba wanzangu wanivumilie, wamekataa.”

Leave A Reply