Kisa Waarabu, Ridhiwani Amvaa Manara

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

 

MWANACHAMA wa Klabu ya Yanga na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amemvaa Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara kwa kumtaka aache siasa kuelekea katika mechi yao dhidi ya JS Saoura ya Algeria na badala yake asubirie dakika 90 ziamue.

 

Simba inatarajiwa kushuka dimbani kesho Jumamosi kuvaana na SJ Saou­ra ya Algeria timu ambayo anachezea Mtanzania, Thomas Ulimwengu, wakikutana katika mchezo wa awali wa Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Ridhiwani alisema kuwa Simba ipunguze siasa kuelekea mchezo huu kwa kumtaka Manara apunguze kuzun­gumza sana na badala yake asubiri matokeo uwanjani na kuwataka wajiandae ipasavyo kuhakikisha wa­naibuka na ushindi kuele­kea mchezo huo kwa kuwa ndiyo wawakilishi pekee hapa Bongo.

 

“Nawatakia Simba kila la kheri kuweza kupata ma­tokeo mazuri na kushinda mechi yao ya Jumamosi kwani wao ndiyo wawak­ilishi wetu pekee ambao wamebakia kwa sasa katika michuano ya kimataifa.

 

“Kwanza kabisa naomba wapunguze siasa kuelekea mchezo huu, Manara ame­kuwa akizungumza sana kupitia mitandao ya kijamii hivyo ni vyema akaacha kuongea sana na badala yake asubiri mechi ichezwe na timu iweze kujiandaa vyema kuelekea katika mchezo huo.

 

“Jambo lingine am­balo nimependa ku­washauri Simba ni katika suala hili la vi­ingilio ambapo kuna kiingilio cha shilingi laki moja huku wenye magari yao watatakiwa kuacha hotelini, jambo hili si sahihi siyo watu wote wenye kiasi hicho cha fedha cha kuweza kutoa ili kuingia uwanjani.

 

“Wawaache watu waingie uwanjani wakafurahie mpira kama ilivyokuwa katika michezo iliyopita ikiwemo dhidi ya Nkana ya Zambia watu waliingia wengi na walifurahia, siyo hivyo wa­navyotaka kufanya, utara­tibu kama huo wenzetu Ulaya wanaufanya shabiki ananunua tiketi kwa mwaka mzima.

 

“Waache kufanya maa­muzi ya kukurupuka, uwanjani siku zote hakuna viti vya VIP na badala yake kuna viti vya watazamaji, walizingatie hilo ili kupata mashabiki wengi wataka­okwenda kuishangilia timu yao,” alisema Ridhiwani.

Stori na Khadija Mngwai

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment