Kisa Wasanii, Musukuma Awalipua TRA kwa JPM, Maagizo Mazito Yatolewa – Video

RAIS Dkt John Pombe Magufuli leo Ijumaa, Juni 7, 2019 amekutana na wafanyabiashara watano atano kutoka Wilaya zote 139 nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa, Lengo ni kufahamu changamoto zao na kusikiliza mawazo yao.

 

Akichangia katika mkutano huo, Mbunge wa Geita na Mfanyabiashara Joseph Kashku ‘Musukuma’ amesem; “Natoka jamii ya ufugaji na soko kubwa lipo Comoro, ukinunua ng’ombe Geita kumsafirisha Tsh 4,000 na unalipia ng’ombe ‘Permit’ ya Tsh 2,500 – Unamsafirisha mpaka Pugu, ili umshushe unalipa Tsh. 6,500. Ukiwa unampeleka Comoro inabidi umpeleke Kwara.

 

“Ukifika Kwara, pale kusajili ng’ombe mmoja ni Tsh. 1,500 na akilala hapo anachajiwa Tsh. 1,000 na lazima wakae siku 14 pale – Kisha unalipa ‘Export Permit’ Dola 30, Tsh. 6,500 ya kupeleka bandarini na siku zote ng’ombe hawa tunanenepesha kwa mashudu.

 

“Wafanyabiashara wa ng’ombe Comoro hawanunui tena huku kwetu, wamehamia Madagascar – Ili usafirishe ng’ombe kutoka Geita, inabidi ulipie kibali wanaita ‘Abnormal’ Dola 10 mtandaoni – Wafugaji wa ng’ombe wengi wana simu za tochi, Wanatoa wapi mtandao?

 

“Kuna biashara inafanyika bandarini, kwa akili zangu ndogo huwa najiuliza sana. Inapoingia meli ya mizigo kuna watu wameshapanga hii inaenda ICD (Inland Container Depot) – Bandari yetu ipo tupu, makontena yanagawanywa kwenda ICD. Nashangaa sana.

 

“Rais wewe una hoteli kule Chato, kabla hoteli yako haijajaa wakija watu unawaambia “nenda kule”, utakuwa na akili gani wewe! – Kwanini tunapeleka makontena yetu kwenye ICD wakati bandari yetu iko tupu? Na kule unalipa $40 kwa siku 7 na ukichelewa ni $80.

 

“Tunakushukuru na Waziri amekuwa msikivu kuhusu dhahabu, ila nilikuwa naangalia tu ile rekodi ya mkoa wangu wa Geita ambao ni kinara wa dhahabu – Toka mwezi wa kwanza hadi wa tano tumekusanya kilo 600. Niliongea Bungeni na wewe leo nikueleze.

 

“Ni kwamba hata theluthi ya dhahabu hatujaweza kukusanya maana kwa Geita tunaweza kukusanya tani moja kwa siku – Sasa pengine kuna udhaifu kwa wasimamizi, nakuomba kama unaweza kutoa kikosi kidogo tuu cha Jeshi kizunguke Geita hutakosa tani 1.

 

“Kama ukikosa tani hiyo kwa kutumia Jeshi tena hata wakiwa hawana nguo za Jeshi, mimi nipo tayari kujiuzulu. Hatuwezi kujisifu tumekusanya kilo 600 – Timu ya ulinzi ilikamata kilo 300 aliyekamatwa alikusanya kwa siku ngapi kama sisi miezi 5 tuna kilo 600,” amesema Musukuma.

TAZAMA HAPA

Loading...

Toa comment