The House of Favourite Newspapers

Kisa Wema, Nyerere Amvaa Polepole: Hiki Chama Hujakiunda… Wewe ni Nani?

0
Steve Nyerere.

HEADLINE inayobamba mitandaoni na kwenye vyombo vya ahabri kuanzia jana jioni ni kuhusu Malkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu kuhama Chadema na kutangaza kurudi kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo uamuzi huo umetolewa ufafanuzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akisema CCM haina taarifa za Wema kwani hajafuata taratibu kuanzia kwenye shina la chama na si kupitia mitandaoni.

Chama chetu sio Daladala mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote, ni heri akabaki hukohuko ama akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu,” aliandika Polepole.

Kauli hiyo imemuibua Staa wa Filamu aliyekuwa rafiki wa karibu wa Wema kabla hajahamia Chadema, Steve Nyerere ambaye amemtolea povu Polepole na kuijibu kauli yake hiyo akiandika;

“Hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya.

“Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia” aliandika Steve Nyerere.

MASTAA WAMFUNGUKIA WEMA ISHU YA KURUDI CCM!

TUJIKUMBUSHE: Wema Sepetu Arudisha Kadi ya CCM na Kujiunga na CHADEMA (Video)

KISA WEMA: Polepole, Steve Nyerere Wavaana Vikali! “Tulia CCM Siyo Yako”

Leave A Reply