Kishindo cha Afro B Katika Wo Wo Wo Akiwa na Rich The Kid na Rimzee
STAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B, ameachia video yake mpya ya kibao “Wo Wo Wo (Ebony)” – ikiwa ni kolabo na Mmarekani, Rich The Kid, na msanii wa muziki wa rap nchini Uingereza, Rimzee.
Ni kolabo ya kimataifa kwani inajumuisha mastaa kutoka mabara tofauti ulimwenguni.
Afro B ni raia wa Ivory Coast ambaye kwa Sasa makazi yake yapo nchini Uingereza katika Jiji la London.
Kabla ya kibao hiki, msanii huyo amepata kufanya kazi na mastaa wengine wa muziki wakiwemo, Wizkid, Slim Jxmmi (Rae Sremmurd), DJ Snake, Sukihana na wengineo.
Tangu wakati huo, amepata kuungwa mkono na Billboard, BET, BBC Radio 1, Capital, Hot 97, Power 105 na The Fader, Rolling Stone & NME ++.
“Wo Wo Wo (Ebony)” ni ufunguzi wa safari mpya ya kuhanikiza hadhira yake, mwakani 2024.
“Mambo makubwa yanakuja. Huu ni mwanzo tu. Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwakweli,” anasema Afro B akizungumzia kazi yake hiyo mpya.