The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Kesi ya Rugemarila na Sethi, Mapya Yaibuka Tena

KESI ya kuhujumu uchumi na kuitia serikali hasara ya mamilioni ya pesa, inayowakabili wafanyabiashara maarufu imezidi kugubikwa na utata dhidi ya afya za watuhumiwa wake, James Rugemarila na Habinder Sethi.

 

Baada ya mshtakiwa wa kwanza James Rugemarila kuomba mahakama imruhusu apatiwe matibabu ya ugonjwa wa saratani unaomsumbua, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, hii leo ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa huyo amefanyiwa vipimo na hajakutwa na ugonjwa wa saratani anaoueleza.

 

Taaifa hiyo ilipingwa na wakili wa Rugemarila, Respicious Didas, ambapo alieleza kuwa suala la ugonjwa wa mteja wake upo wazi kwamba ana uvimbe unaoonekana.

 

“”Licha ya ugonjwa wa mteja wangu kuwa wazi, bado upande wa mashtaka haujachukua hatua yoyote kuhusiana na uvimbe huo, linapaswa kupewa kipaumbele na ugunduzi wa ugonjwa wake ufanyike kwa kutumia madaktari wa India”, amesema Wakili Didas.

 

Pamoja na hayo Wakili huyo ameendelea kuelezea kuwa mteja wake aliwahi kuugua saratani na kufanyiwa upasuaji mwaka 2008, na kwamba ugunduzi huo pamoja na matibabu yote, vilifanyika nchini India, baada ya vipimo vilivyokuwa vinafanyika hapa nchini vilikuwa vina shida, na ndio sababu aliamua kuanzisha kituo cha saratani hapa kwa ajili kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi, waweze kupata matibabu katika kituo chake.

 

Kwa upande wa mshtakiwa mwengine  ametakiwa kufanyiwa upasuaji wa kutoa puto lililpo tumboni mwake linalodaiwa kuwa limeisha muda wake, kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, chini huku madaktari wake waliokuwa wakimtibia awali kutoka nchini Afrika Kusini  wakiwepo pia.

Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo ameutaka upande wa mashtaka kusimamia matibabu ya watuhumiwa hao Rugemarila pamoja na Seth, na kuahirisha kesi hiyo mpaka Februari 2, 2018.

BREAKING: HATIMAYE CHADEMA WARUDI KWENYE UCHAGUZI, WACHUKUA FOMU

Comments are closed.