The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Mbowe na Wenzake Wafikishwa Mahakamani kwa Dhamana

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzanke watano wa chama hicho wameshafikishwa katika Mahakama ya Kisutu wakisubiri shughuli za kimahakama kuanza ili wakamilishe masharti ya dhamana. Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wamekusanyika nje ya Mahakama wakiwasubiri viongozi wao.

 

Mnamo March 29, 2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamru Mbowe na wenzake wapewe dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh milioni 20, kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao wa vijiji au mtaa na kuwa, nakala za vitambulisho vyao na kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kila Alhamisi kisha.

 

Dhamana hiyo ilishindikana kutokana na magereza kutowafikisha watuhumiwa hao mahakamani hapo hivyo hivyo kushindwa kusaini hati za dhamana zao na kushindwa kutimiza masharti hayo kwa kile kilichodaiwa gari lililokuwa liwapeleke mahakamani lilikuwa bovu.

 

Lakini pia baada ya kutolewa dhamana wakili wa serikali aliwasikisha notice ya kupinga dhamana hiyo na upande wa utetezi ukatoa hoja zake za kukataa notice hiyo ambapo baada ya kusikikiza hoja za pande zote, hakimu Mashauri aliamua notice hiyo isijadiliwe na kuitaka Jamhuri kama inapinga dhamana hiyo iwasilishe notice baada ya watuhumiwa kusaini hati zao za dhamana.

 

Mahakama iliamua Mbowe na wenzake wafikishwe mahakamani hapo leo Jumanne, Machi 3, kutimiza masharti ya dhamana yao ili waachiwe.

 

Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe.

Comments are closed.