The House of Favourite Newspapers

KISUTU: RCO, ILALA AULIZWA KAMA ANAPAFAHAMU ANAPOISHI RAIS MAGUFULI

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (kushoto) akiwa na mama yake wakati akishuka ngazi baada ya kusikiliza kesi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2018.
Taswira ilivyoonekana katika lango kuu la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi hiyo kuahirishwa.

MKUU wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hajawahi kumuhoji Rais Dkt. John Joseph Magufuli jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kawe Halima Mdee dhidi yake.

 

Msangi ameyaeleza hayo leo mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akijibu swali la Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.

 

Katika kesi hiyo, Mdee anakabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya uchochezi’ ‘Chafu’ kwa Rais Magufuli.

 

Akimuhoji shahidi huyo, Wakili Kibatala alimuuliza Msangi kama anamfahamu Rais  Magufuli na anaishi wapi. Ambapo alijibu kuwa anaishi Ikulu akamuuliza tena  shahidi huyo kama aliwahi kwenda kumuhoji jinsi anavyojisikia kuhusu maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mdee kwa sababu yeye ndiye muhanga.

 

Msangi akijibu swali hilo aliieleza kwamba hajawahi kwenda kumuhoji wala hakutumia taratibu zozote za kumuhoji.

 

Msangi akiendelea kueleza katika  ushahidi wake amedai kuwa hafahamu msimamo wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Rais Magufuli kuhusu watoto wa kike waliopata mimba shule wasirudishwe shule.

 

Pia RCO Msangi alipoulizwa kwamba Mdee alikaa muda gani chini ya ulinzi, amedai kwamba  siyo kwa zaidi ya Saa  48.

 

 

Baada ya shahidi huyo kumaliza kuhojiwa na Wakili Kibatala, Hakimu Simba amesema kesi hiyo imetimiza mwaka mmoja na ilipaswa iwe ishatolewa hukumu, na hivyo akaiahirisha  kesi hiyo hadi  Agosti 7 mwaka huu ili kuendelea na ushahidi.

Comments are closed.