The House of Favourite Newspapers

Kitale: Uteja una mwisho wake

0

DSC_1545Mkali wa vichekesho nchini, Musa Kitale ‘Mkude Simba’.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

MKALI wa vichekesho nchini, Musa Kitale ‘Mkude Simba’ amefunguka kuwa siku zote amekuwa akipenda kuigiza kama mtu anayetumia madawa ya kulevya, anaamini kuwa itafika kipindi atakuja na mtindo mwingine ambao utakuwa gumzo zaidi.

Akizungumza na Mikito Jumatano, Kitale alisema amekuwa akitumia mtindo huo kwa ajili ya kutoa somo kwa vijana wa Kitanzania namna vijana wanavyoathirika na utumiaji wa madawa hayo huku akiamini kwamba itafika wakati atalazimika kuwa na kitu kipya.

“Unajua jamii yetu imeathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya, sasa kuigiza kwangu katika hali ya uteja ni sehemu ya kutoa somo kwa vijana ili watambue kuwa madawa ya kulevya si kitu kizuri kwa sababu yanakufanya ushindwe kufanya mambo mengi katika maisha yako.

“Lakini kila mtindo una mwisho wake ingawa uteja ndiyo umenifanya nifahamike zaidi, ila itafika wakati nitabadilika ili niweze kuendana na kasi itakayokuwepo,” alisema Kitale.

Leave A Reply