Kitawaka Simba SC vs Yanga SC Kesho

 

WAKATI Simba Queens na Yanga Princess wakitarajia kuvaana kesho Jumapili, makocha wa timu hizo wametambiana kila mmoja kuondoka na ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

 

Katika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kiingilio kimetangazwa kuwa ni Sh 2000 tu. Wakizungumza na Championi Jumamosi, makocha hao walisema maandalizi yao yapo vizuri na lengo ni kuona wanapata ushindi na kuwa kwenye nafasi nzuri.

Kocha wa Simba, Omary Mbweze, alisema: “Simba tumejipanga vizuri kushinda kila mechi, nawaheshimu Yanga, tayari nimewaona na ninajua mapungufu yao, lakini siwezi kuwadharau, zaidi nahitaji pointi tatu.

 

Kwa upande wa Kocha wa Yanga, Hamis Kinonda, alifunguka kuwa: “Lengo ni sisi kushinda ingawa tumekuwa tukipambana licha ya ugeni kwenye ligi, tunajua wenzetu wana wachezaji wenye uzoefu tofauti na sisi, lakini tutapambana kupata ushindi.”

 

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Soka la Wanawake, Amina Karuma, alisema wamejipanga na ulinzi utakuwa wa kutosha pamoja na burudani zikiongozwa na wadhamini wao Serengeti Lite, hivyo mashabiki wajitokeze kushuhudia mchezo huo.

Martha Mboma na Ibrahim Mussa

Loading...

Toa comment