Kitawaka Waliooa na Wasiooa Leo Uwanja wa Kenton, Sinza
KAMPUNI ya Euromax wanaotengeneza kinywaji cha Smart Gin na Kampuni ya Creative Bee kwa pamoja wamekabidhi jezi za mchezo wa Waliooa na Wasiooa kwa wafanyakazi wa Global Group unaotarajiwa kupigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja shule ya Kenton Iliyopo Afrikasana, Dar.
Kinywaji cha Smart Gin na Creative Bee ndiyo wamedhamini mchezo huo kwa upande wa vifaa vya michezo.Jezi hizo za timu zote mbili zilikabidhiwa jana katika kipindi cha michezo cha Krosi Dongo kinachorushwa mubashara na +255 Global Radio na Global Tv Online.
Aidha, Kampuni ya Tukuyu Spring Water inayojishughulisha na uzalishaji maji ya kunywa jana pia ilikabidhi maji katoni 17.Mbali ya hapo, Kampuni ya Tukuyu imeahidi kutoa fulana maalumu kwa timu ya Wasiooa.