The House of Favourite Newspapers

Kitengo Cha Usalama Barabarani, BETPAWA Watoa Mafunzo Kwa Bodaboda 250 Dar

0
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Deus Sokoni akiwapa somo waendesha bodaboda. 

Dar es Salaam, 5 Septemba 2023: Madereva 250 wa pikipiki maarufu kama bodaboda wamepata mafunzo maalumu ya kuwakumbusha sheria na kanuni za usalama barabarani pamoja na kupatiwa vifaa ikiwemo kofia ngumu ambazo zitawakinga dhidi ya ajali za barabarani.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mafunzo hayo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Deus Sokoni ambaye pia ni Mwalimu wa somo la usalama barabarani nchini na duniani amesema, mafunzo hayo kwa madereva wa pikipiki wanaosafirisha abiria kibiashara maarufu kama bodaboda yamelenga kuwakumbusha sheria za usalama barabarani juu ya maisha yao wenyewe, uadilifu katika biashara zao pamoja na kutimiza wajibu wao ili wapate haki zao.

Amesema  hayo kwa kushirikiana na kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa ambao wamedhamini mafunzo hayo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania, Borah Nganyungu.

“Msingi waliouona BetPawa katika biashara zao za kufanya betting kundi kubwa wanaoshiriki ni hili la waendesha pikipiki, wanafanya betting hadi katika maisha yao kupitia vyombo vyao vya moto na sisi kama jeshi la Polisi tunasimamia usalama wa raia na mali zao na dawati la usalama barabarani tunalinda usalama wa watumiaji wa barabara.” Amesema.

Pia ameeleza, amewataka madereva hao kuhakikisha wanakuwa na leseni pamoja na bima kwa vyombo vya moto wanavyoendesha pamoja na kuvaa kofia ngumu wao binafsi na abiria. Aidha amewaelekeza madereva hao kufuata sheria na kanuni za barabara ikiwemo alama za barabarani.

“Pia kuna madereva pikipiki wanaendekeza ulevi, waache pombena vilevi vingine kwa imani ya kuongeza munkari…Hii hapana pombe sio soda, pombe sio maji inapelekea kifo kwa hiyo tunawaelimisha waenda pikipiki wabeti kwa msingi wa kutafuta maisha sio kwa msingi wa kushindana kijinga barabarani.

Martin Kayanda dereva bodaboda aliyehudhuria mafunzo hayo akizungumza na vyombo vya habari.

“Wabeti kwa kuwashirikisha wamiliki wa vyombo kwa kuhakikisha wanabeti na dereva mwenye leseni, bima ili wabeti kihalali barabarani katika kutafuta pesa.” Amesema.

Pia amesema kupitia BetPawa wajiendeleze kijasiriamali kwa kutengeneza kesho bora kiuchumi na sio kubeti na  uhai wao kwenye vyombo vya moto.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetPawa Tanzania, Borah Nganyungu amesema wameungana na kitengo cha kutoa elimu ya usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki wanaosafirisha abiria kibiashara.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kama Kampuni ya michezo ya kubashiri tunarudisha kwa jamii kwa njia moja au nyingine na kwa kuanza na hili leo tutatoa kofia ngumu kwa bodaboda 250 walioshiriki mafunzo.” Amesema.

Pia amesema kuwa kampuni hiyo itawafikia bodaboda wengi zaidi katika mikoa mingine ili kutoa mafunzo ya kujikinga dhidi ya elimu ya barabarani.

‘Tafiti zinaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa la ajali barabarani huku mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza, tumeanzia hapa kusaidia kutoa mafunzo ya usalama barabarani na kuwapatia vifaa vya kuwalinda dhidi ya ajali za barabarani.” Amesema.

John Kinyonga mmoja wa dereva bodaboda ameshukuru kwa kutolewa kwa mafunzo hayo ya kujikinga dhidi ya ajali hususani katika maeneo ambayo ajali inaweza kuepukika.

Amewataka madereva wa vyombo hivyo vya moto kushiriki mafunzo ya namna hiyo na kuziomba kampuni nyingine za namna hiyo kuwafikia madereva wengi zaidi na kuwapa mafunzo zaidi ili kupunguza ajali.

Pia Martin Kayanda dereva bodaboda kutoka kituo cha Machinga Complex amesema anaishukuru kampuni ya BetPawa kwa kuwapa mafunzo ya usalama barabarani na kuwakumbusha madereva wa bodaboda kutumia mafunzo hayo kwa kujiepuesha na kuwaepusha wengine dhidi ya ajali za barabarani.

Leave A Reply