The House of Favourite Newspapers

Rais Ruto Amteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki

Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang’ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa Ijumaa.

Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais kuhusu uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kujaza nafasi katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya,” Wetang’ula alitangaza.
Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo. Pia hakuna sharti la kura ya thuluthi mbili.

AHMED ALLY – SIMBA vs YANGA – ”TUTAWAFANYA VIBAYA MNOOO – TUMEDHAMIRIA KUWAKAANGA”….