The House of Favourite Newspapers

Kitokololo Aitosa Fm Academia

0

kitokololo

Kalidjo Kitokololo

Richard Bukos

RAPA aliyeji-zolea umaarufu katika Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma,’  Kalidjo Kitokololo ameitosa rasmi bendi hiyo na kutimkia Bendi mpya ya BMM Ngwasuma.

Akizungumza na Showbiz Xtra hivi karibuni katika onesho la BMM Ngwasuma lililofanyika Meeda, Sinza  jijini Dar, Kitokololo alisema ameamua kuachana na bendi hiyo aliyoitumikia muda mrefu baada ya kumaliza mkataba wake na kuamua kutafuta masilahi zaidi.

“Si unajua muziki mimi ndiyo kazi yangu, hivyo nimeamua kujiunga na BMM Ngwasuma chini ya Prezidaa Mulemule kufuata masilahi zaidi vilevile naona kabisa ikiendelea na uongozi uliopo hivi sasa ni lazima itishe na kuzifunika bendi zote zilizotagulia,” alisema Kitokololo.

Leave A Reply