The House of Favourite Newspapers

Kituo cha Masaji Chafungiwa na Serikali, Mmiliki Atozwa Faini

0

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imechukua hatua kadhaa ikiwemo kukifungia kituo kimoja cha masaji kikichopo Nzasa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Waziri Dkt. Doroth Gwajima, imekuja baada ya video ya tangazo la huduma za masaji iliyowekwa mitandaoni, kuripotiwa kuwa ina vitendo vilivyo kinyume na maadili.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imeeleza kuwa huduma za kituo zimesitishwa kuanzia Oktoba 26, 2023 kutokana na kutokidhi vigezo vya Sheria Namba 23 ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, pia mmiliki ametozwa faini ya Tsh. 500,000 pamoja na kupewa maelekezo mengine ambayo kama atayakiuka atafikishwa mahakamani.

Pia Waziri Gwajima ameelekeza mamlaka husika kuwafuatilia watoa huduma wengine ili kuwabaini wasiotimiza matakwa ya sheria ikiwemo kuathiri ustawi wa jamii na kuchochea mmomonyoko wa maadili unaosababisha matukio ya unyanyasaji, udhalilishaji wa kijinsia ambapo waaathirika wakuu ni watoto.

Aidha, Wizara imetoa mawasiliano ya moja kwa moja kwa wanaotaka kuripoti masuala mbalimbali Wizarani watumie namba 0734 986503 na 026 2160250, matukio ya Ukatili wa Watoto namba 116 Saa 24 kila siku bila malipo. Na iwapo Waziri mwenye dhamana atahitajika, tuma ujumbe kwenye namba 0765 345777 na 0734 124191.

Leave A Reply