The House of Favourite Newspapers

Kiungo Azam Afuzu kukipiga Liverpool

0

KIUNGO kinda wa Azam FC, Khelffin Hamdoun, amefanikiwa kufuzu majaribio katika timu ya vijana ya Liverpool.

Hamdoun alienda mjini Liverpool, England mwezi uliopita ambapo alifanya majaribio na kufanikiwa kufaulu lakini ilishindikana kuingizwa kwenye usajili kutokana na dirisha kufungwa.

Kwa sasa bado yuko Liverpool na muda wowote kuanzia sasa anatarajia kurejea Bongo kujiunga na Azam.

Akizu

ngumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema kuwa: “Ni kweli Khelffin yupo Liverpool kwa ajili ya majaribio, ameweza kupita lakini shida imekuja usajili wa Liverpool umeshafungwa.

“Atarejea nyumbani mpaka usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa, Inshaallah ataenda tena.”

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave A Reply