KIWANJA CHA MIL. 97 CHA SANCHI CHAZUA GUMZO
MUDA mfupi mara baada ya kuanika kiwanja anachodai kukinunua kwa shilingi milioni 97 maeneo ya Bunju jijini Dar, mwanamitindo Jane Rimoy ‘Sanchi’ amezua gumzo kwa mashabiki wake mitandaoni.
Sanchi aliweka picha yake mtandaoni ikimuonesha akiwa amesimama katika kiwanja hicho ambacho aliiambia Star Showbiz ya Uwazi kuwa ni muunganiko wa viwanja viwili na bei yake ni milioni 97.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mashabiki wengi walizua gumzo kwa kuongelea umbo lake huku wengine wakiwasihi wadada wengine waige mfano.“Kumbe ukiwa na umbile kubwa unalipa, cheki anamiliki kiwanja,” ilisomeka moja ya komenti. Kuna haja ya kupata kiwanja Bunju niwe jirani yako nifaidi kwa macho,” ilisomeka komenti nyingine
STORI: IMELDA MTEMA
Comments are closed.