The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kizimbani kwa Kufungua Simu Zilizofungwa na TCRA

0

WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujihusisha na kufungua simu zilizofungwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kubadili uhalisia wa IMEI namba.

 

Wakisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Esther Martin, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mbando, watu hao, Abdul Nassor na Said Msangi, ambao ni mafundi simu wa Kariakoo, Dar es Salaam, wanadaiwa kuwa Februari 27, mwaka huu walibadili namba tambulishi (maarufu IMEI) ya simu aina ya Tekno.

 

TCRA ilifunga simu zote bandia na zile ambazo hazikufikia viwango vya kutumika nchini (simu feki).

 

 

Leave A Reply