The House of Favourite Newspapers

Kizza Besigye Kupandishwa Kizimbani Kwa Uhaini Leo

0

kizza-besigye-campaigns-jinja-uganda

Kizza Besigye.

KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye asubuhi hii anatarajiwa kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za uhaini.

Kizza Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.

Inaonekana leo itakuwa ni nafasi nzuri kwa upande wa mashtaka kurekebisha makosa katika hati za mashtaka dhidi ya Kizza Besigye ambapo itakuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini kwani awali alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika mji huo wa Moroto.

Kiiza

Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku shughuli za mahakama zikiwa zimefungwa.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.

Besigye anakabiliwa na tuhuma za kujitangaza kuwa mshindi wa urais wa Uganda mwezi Februari japo mshindi aliyetangazwa na mahakama ya juu nchini Uganda ni Rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa wiki iliyopita kuwa Rais wa Uganda.

Credit: BBC

Leave A Reply