The House of Favourite Newspapers

Klabu ya Chelsea Imetangaza Kukamilisha Dili la Kumsajili Cucurella Kutoka Brighton

0
Marc Cucurella amekamilisha usajili wa kujiunga na Chelsea

KLABU ya Chelsea imetangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto wa klabu ya Brighton and Hove Albion raia wa Hispania Marc Cucurella kwa ada ya usajili wa paundi milioni 62.

 

Katika dili hilo kinda wa klabu ya Chelsea Levi Colwill naye ataelekea upande wa pili kwa mkopo wa msimu mzima ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa Cucurella.

Cucurella amesajiliwa kwa ada ya jumla ya paundi milioni 62

Kabla ya kujiunga na Chelsea Cucurella alikuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester City ingawa ada ya uhamisho ya paundi milioni 50 ilionekana kuwa kiasi kikubwa ambacho Manchester City hawakuwa tayari kutoa.

Utambulisho wa Marc Cucurella

Kuongezeka kwa Cucurella kunatoa unafuu kwa beki mwenzie ambaye ni raia wa Uingereza Ben Chilwell kutokuwa na presha kubwa sana katika kikosi hicho ukilinganisha ametoka kwenye majeruhi ya muda mrefu, na tayari kocha wa Klabu hiyo Thomas Tuchel amesisitiza kuwa itamchukua muda kurejea katika ubora wake na hatakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Everton.

Leave A Reply