The House of Favourite Newspapers

Klabu ya Yanga Yamtangaza Lomalisa Kama Mchezaji Wao Mpya Kuelekea Msimu Ujao

Joyce Lomalisa Mutambala Beki mpya wa klabu ya Yanga raia wa Congo DR

KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi mchezaji mwingine wa kimataifa raia wa Congo DR, Joyce Lomalisa Mutambala kuwa mchezaji wao kwa mkataba wa miaka miwili hadi 2024 ambaye ataanza kuwatumikia Wananchi kuanzia msimu ujao.

Mutambala amewahi kuichezea klabu ya AS Vita ya nchini Congo

Mutambala (29) anayecheza nafasi ya beki wa kushoto amewahi kucheza timu mbalimbali Barani Afrika na Ulaya ikiwemo AS Vita ya nyumbani kwao Congo, Royal Excel Mouscron ya Ubelgiji, GD Interclube Luanda ya Angola na FC Onze Bravos do Maquis ya Angola.

Lomalisa raia wa Congo DR

Yanga tayari imeshasajili nyota watano wa Kimataifa na ambao weshatambulishwa mpaka sasa ni; Lazarous Kambole, Bernard Morrison, Gael Bigirimana, Joyce Lomalisa Mutambala na amesalia Stephanie Ki kutambulishwa na kufunga ukurasa wa usajili wa Kimataifa kwa Yanga msimu huu.