The House of Favourite Newspapers

Klopp: Tunapita Kwenye Mateso Makubwa Uwanjani

0

KUPOTEZA kwa kichapo mbele ya Fulham kumemfanya Kocha Mkuu wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, aweke wazi kuwa mateso ambayo wanapitia kwa sasa ni makubwa kwa kukosa matokeo ndani ya uwanja.

 

 

Liverpool wakiwa Uwanja wa Anfield ubao ulisoma Liverpool 0-1 Fulham na bao lilifungwa na Mario Lemina dakika ya 45.

 

 

Matokeo hayo kwa Liverpool yanawafanya wazidi kuwa kwenye wakati mgumu wa kutetea taji lao kwa msimu huu wa 2020/21 kwa kuwa wapo nafasi ya 8 na pointi zao ni 43 baada ya kucheza jumla ya mechi 28.

 

 

 

Wapinzani wao Fulham wapo nafasi ya 18 na pointi zao ni 26 kibindoni wote pia wamecheza jumla ya mechi 28 ndani ya Ligi Kuu England ambayo imekuwa na ushindani mkubwa.

 

 

Klopp amesema: “Haya maumivu ambayo tunapitia kwa sasa inatosha kwani matokeo yamekuwa siyo mazuri, ninaamini kwamba tutarejea kwenye ubora wetu hivi karibuni,” alisema.

Leave A Reply