The House of Favourite Newspapers

Klopp Amkingia Kifua Trent Alexander-Arnold Baada ya Kuachwa Timu ya Taifa

0
Trent Alexander Arnold

KOCHA Mkuu wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza Jurgen Klopp amemkingia kifua mlinzi wa kulia wa klabu hiyo na raia wa Uingereza Trent Alexander Arnold baada ya kuachwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza Gareth Southgate katika kikosi cha wachezaji wa kuwakilisha timu ya Taifa katikla mkichezo iliyopita ya Uefa Nations League.

 

Trent alipigwa benchi katika mchezo dhidi ya Italy ambao Uingereza ilipoteza kwa bao 1-0 lakini pia akaondolewa kabisa kwenye kikosi kwenye mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Ujerumani uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 3-3.

Trent Alexander Arnold akiwa na Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp

Lakini Kocha Mkuu wa Liverpool ameibuka na kusema kuwa Trent ni mchezaji ambaye bado ana wakati wa kujifunza katika idara ya ulinzi lakini ni aina ya mchezaji ambaye katika timu yoyote ambayo anaweza kupata nafasi ya kufanya kazi basi atamsajili mara moja kwani ubora wake katika idara ya ushambuliaji ni wa kiwango cha juu sana,

 

“Kiukweli ningeamua tofauti kabisa lakini sipo kwenye nafasi hiyo.

“Mtazamo wangu ni chaguo rahisi, timu yoyote ambayo naweza kuifundisha kwa sasa naweza kumsajili kwasababu ana balaa.” amesema Klopp.

Reece James

Mlinzi wa kulia wa klabu ya Chelsea Reece James amekuwa akipewa kipaumbele zaidi ya Trent Alexander Arnold kutokana na uwezo wake wa kukaba lakini pia kusaidia mashambulizi dhidi ya timu pinzani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply