The House of Favourite Newspapers

KMC Yaipiga Mkwara Polisi Tanzania

0

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa unahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zake zote za Ligi Kuu Bara na itaanza kufanya hivyo mbele ya Polisi Tanzania.

Septemba 29, KMC itakuwa na kazi mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi na jana kikosi kiliibukia huko Moshi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa wanatambua kwamba ligi inaanza na wana malengo ya kufanya vizuri hivyo wataanza kufanya hivyo mbele ya Polisi Tanzania.

“Kuanza kwa ligi kwetu sisi ni maandalizi na mwanzo mzuri ni jambo ambalo tunalihitaji hivyo tutaanza kufanya mbele ya Polisi Tanzania, maandalizi ambayo tumeyafanya ni makubwa na tunaamini tutafanya vizuri.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa nasi, hatutawaangusha na tutaendelea na pira letu lile, pira spana na pira kodi na kwa usajili ambao tumefanya ni moto wa kuotea mbali,” alisema.

Nyota ambao ni wapya ndani ya KMC ni pamoja na Faroukh Shikalo ambaye alikuwa anakipiga Yanga pamoja na Miraj Athuman aliyekuwa anacheza Simba.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply