KMC YAONDOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO, YAPIGWA 2-1 NA AS KIGALI
Timu ya KMC leo Agosti 23, 2019 imekuwa ya kwanza kutoka Tanzania kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa AS Kigali katika mtanange uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Rwanda timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana hivyo imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1.
AS Kigali wapita bao la kwanza dakika ya 28 kupitia kwa Rashid Kalisa baada ya mlinzi mmoja wa KMC kufanya makosa wakati wa kuokoa na kuwafanya Wanyarwanda hao kutengeneza shambulizi lililozaa bao.
Bao hilo lilidumu mpaka timu hizo zinaenda mapumziko ambapo kipindi cha pili KMC waliwaingiza Vitalis Mayanga, Mohammed Samata na George Sangija ambao waliongeza kasi katika idara ya ushambuliaji.
Dakika ya 64 Erick Nsabimana aliifungia AS Kigali bao la pili baada ya kupokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja huku walinzi wa KMC wakidhani alikuwa ameotea.
Comments are closed.