The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga Aiweka Kando Kariakoo Dabi Ligi Kuu Bara

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.

KOCHA Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema kuwa haufahamu mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao wa Kariakoo Dabi badala yake anaifahamu michezo miwili dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.

Miloud alisema kuwa maandalizi yake ya michezo ya ligi ameielekeza kwa timu hizo mbili na siyo dhidi ya Simba ambayo haipo katika ratiba zake.

“Ninafahamu tumebakisha michezo miwili ya ligi pekee dhidi ya Prisons na Dodoma Jiji ambayo itaamua hatima ya ubingwa wetu ya ligi, hivyo siutambui mchezo huo wa dabi kama kocha,” alisema Miloud.

Stori na Wilbert Moland, GPL