The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha Amkomesha Tshishimbi, Amleta Kiboko Yake Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amepanga kushusha kiungo mmoja mkabaji wa kimataifa atakayecheza namba sita baada ya kugundua upungufu katika safu hiyo.

 

Safu hiyo ya kiungo hivi sasa inachezwa na Mkongomani, Papy Tshishimbi na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambao kocha ameonekana akiwatumia katika michezo mbalimbali ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA msimu huu.

 

Kati ya viungo wanaotajwa kutua Yanga ni kiungo wa Nkana Rangers ya Zambia, Musa Mohamed ambaye mwenyewe alithibitisha kupitia kwenye moja ya mtandao wa nchini humo kuwa kwenye mazungumzo na Yanga iliyoonyesha nia ya kumsajili.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael alisema kuwa anaamini uwezo wa viungo alionao Yanga, lakini ni lazima asajili kiungo mmoja anayeimudu vema nafasi hiyo ya kiungo huyo atakayeanzisha mashambulizi kuanzia chini kwenda juu.

 

Eymael alisema kuwa viungo alionao, Tshishimbi na Fei Toto wenyewe wana tatizo la kuhama katika maeneo yao na kusababisha kuwapa mzigo mzito mabeki wa kati kutokana na makosa yao.Aliongeza kuwa katika kupunguza makosa hayo ni lazima alete kiungo atakayemudu kucheza nafasi hizo zaidi ya Tshishimbi na Fei Toto ambao hao atawapa majukumu mengine ya uwanjani.

 

“Msingi wa timu siku zote unaanzia chini, nikimaanisha namba sita ambaye kama yeye akishindwa kutimiza majukumu yake vizuri, basi lazima makosa yatakuwa mengi golini kwetu.

 

“Kama umekuwa ukifuatilia mechi ambazo tumekuwa tukipoteza makosa mengi yamekuwa yakifanywa na viungo wakabaji namba sita wamekuwa hawatimizi vema majukumu yao ya uwanjani.

 

“Hivyo, basi nimepanga kusajili kiungo mkabaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi hiyo ya kiungo ambaye hatakuwa akihama katika eneo lake la katikati, tayari nipo kwenye mazungumzo na baadhi yao kutoka mataifa mbalimbali ambayo nisingependa kuweka wazi kwa hivi sasa,” alisema Eymael

Stori: Wilbert Molandi,Dar

Leave A Reply