Kocha JKT Queens awaponda waamuzi

LICHA ya kupata ushindi ugenini dhidi ya Tanzanite, Kocha wa JKT Queens, Ally Ally, amewatupia lawama waamuzi waliochezesha mchezo huo kwa kuwabeba sana wapinzani wao na kusababisha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao machache.

 

Mchezo huo wa mzunguko wa pili katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa ambapo JKT Queens waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Asha Mwalala dakika ya 69 na Fatuma Mustapha dakika ya 90.

 

Alisema timu ya Tanzanite iliwashinda tu kwa upande wa waamuzi na si kwamba ni timu bora kwani mzunguko wa kwanza waliweza kuwatandika mabao 6-0, hivyo matarajio yao mzunguko wa pili kuibuka na ushindi mnono zaidi. “Ligi ni kubwa lakini waamuzi wanaochezesha hawajui kuchezesha soka.

 

Naiomba TFF kuwapanga waamuzi ambao wanachezesha kwa haki ili kutoharibu ladha ya ligi hii,” alisema Ally.

Toa comment