The House of Favourite Newspapers

Kocha Kaze aihofia Namungo

0

CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa anatambua ubora wa wapinzani wake Namungo FC ambao atakutana nao, Novemba 22, Uwanja wa Mkapa jambo ambalo limemfanya atafute mbinu ya kupata matokeo kwenye mchezo huo.

 

Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 24, inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya tisa na pointi 14 zote zikiwa zimecheza mechi 10 ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.

 

Kaze mwenye tuzo ya kocha bora kwa mwezi Oktoba anakutana na Namungo FC ambayo msimu uliopita chini ya kocha Hitimana Thierry kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa waligawana pointi mojamoja baada ya sare ya kufungana mabao 2-2.

 

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaze alisema kuwa wapinzani wake wapo vizuri licha ya kutokuwa na mwendo unaofurahisha kwa upande wao.

 

“Ukizungumzia Namungo ni moja ya timu ambazo zinafanya vizuri, niliona kwa msimu uliopita namna ilivyokuwa kwenye ubora, ila kwa sasa naona mambo yamekuwa tofauti lakini haina maana kwamba haipo vizuri.

 

“Tutaingia ndani ya uwanja kusaka pointi tatu na nimewaambia wachezaji kwamba wanatakiwa kuwaheshimu wapinzani wetu kwani ni timu nzuri,” alisema Kaze.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply