The House of Favourite Newspapers

Kocha Mcongo naye atimka Yanga SC

 Kocha msaidizi Mkongomani, Guy Bukasa

IMEFAHAMIKA kuwa kocha msaidizi Mkongomani, Guy Bukasa, aliyetua nchini kwa ajili ya kuifundisha Yanga ametimka kimyakimya kwenye klabu hiyo na kurudi nyumbani kwao DR Congo.

 

Kocha huyo, alitua nchini wiki mbili zilizopita na kuanza kibarua cha kuki­noa kikosi hicho kwa ajili ya Kombe la Shirikisho Afrika akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa aliyemaliza mkataba wa kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezi­pata Championi Jumatano, kocha huyo aliondoka nchini baada ya kushindwa kufikia muafaka masuala ya kimkataba na viongozi wa Yanga kabla ya kubeba mabegi yake na kurudi kwao.

 

Mtoa taarifa huyo alisema, kocha huyo ana wiki mbili tangu ameondoka kwenye timu hiyo iliyokuwa inajifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

 

“Nashangaa kuona hadi sasa mme­kuwa kimya, kocha Mcongo aliyekuja kuwa msaidizi wa Zahera sasa ni wiki mbili hayupo hapa nchini.

 

“Hivyo, kocha Zahera hivi sasa yupo peke yake anakinoa kikosi hicho aki­shirikiana na kocha wa viungo Mwandila (Noel), baada ya kuondoka huyo mpya.

 

“Kikubwa kocha huyo alishindwa kufikia muafaka mzuri na mabosi wake hao ya kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Zahera kuzungumza ku­zungumzia hilo alisema kuwa :“Sifahamu taarifa za kuondoka Yanga kwa kocha huyo, nilikuwa naye kwa kipindi fulani, lakini siku za hivi karibuni sijamuona uwanjani.”

Comments are closed.