The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu Simba amtaja Emmanuel Okwi

0

Dylan-Kerr

Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr.

Wilbert Molandi na Sweetbert Lukonge
KOCHA Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amemkumbuka mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mganda, Emmanuel Okwi na kutamka kuwa kama angempata nyota huyo, basi tatizo la ushambuliaji lingemalizika Msimbazi.

Kauli hiyo, aliitoa jana mara baada ya kumalizika mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mganda huyo, aliihama timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu uliopita na kwenda SonderjyskE Fodbold ya Denmark.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kerr alisema kuwa anamjua vizuri mshambuliaji huyo kupitia mitandao mbalimbali, hivyo anakijua vyema kiwango chake cha ndani ya uwanja.

Muingereza huyo alisema, mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo anaamini kama angekuwepo kwenye kikosi chake basi angemaliza tatizo hilo la ufungaji.

“Nikiwa hapa naifundisha Simba nilipewa taarifa za Okwi na kuanza kumfuatilia kwenye mitandao, pia kwenye klabu yake mpya anayoichezea ya huko Denmark.

“Akiwa huko anaisaidia timu yake hiyo mpya kwa kufunga mabao, ninaamini kama angekuwepo Simba angetusaidia sana kwa maana washambuliaji wangu wanapoteza nafasi nyingi katika kufunga mabao.

“Lakini hata hivyo siwezi kuwalaumu viongozi kumuuza Okwi Denmark, kwa sababu mchezaji anaangalia maslahi,” alisema Kerr.

Leave A Reply